Ijumaa 13 Machi 2026 - 22:22
Siku ya Qudsi ni siku ya kutangaza amani duniani

Hawza/ Kiongozi wa Jumuiya ya Shia Ithnaasharia Tanzania (TIC), Sheikh Hemedi Jalala, leo hii katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Qudsi Duniani, amesema kuwa; lengo kuu la siku hii ya Qudsi ni kulinda amani, umoja na mshikamano. Amesisitiza kuwa; ni haki kwa kila mtu anayependa amani duniani kujitokeza katika siku hii kwa ajili ya kulinda uhuru na haki ya kila mwanadamu, bila kujali tofauti za dini, taifa au rangi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Qudsi Duniani yaliyofanyika ulimwenguni kote leo hii, Tanzania nayo haikuwa nyuma katika kuungana kwa dhati na Waislamu wenzao wanaoteseka wa Palestina. Katika maadhimisho hayo, Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithnaasharia Tanzania, Mawlana Sheikh Hemedi Jalala, alitoa khutuba yenye kugusa hisia na nafsi za wasikilizaji, ambapo aligusia nukta mbalimbali zilizohusiana na dhulma na mateso wanayoyapitia watu wa Palestina.

Katika hotuba yake, huku akianza kwa aya tukufu isemayo:

{ سُبحَـٰنَ ٱلَّذِیۤ أَسرَىٰ بِعَبدِهِۦ لَیلا مِّنَ ٱلمسجدِ ٱلحَرَامِ إِلَى ٱلمسجِدِ ٱلأَقصَا ٱلَّذِی بَـٰرَكنَا حولَهُۥ لِنُرِیَهُۥ مِنۡ ءَایَـٰتِنا إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِیعُ ٱلبَصِیرُ }


[Surah Al-Isrāʾ: 1]

Alisema: Aya hii inazungumzia jambo la Qibla cha kwanza cha Waislamu na Msikiti mtakatifu uliopo katika nchi ya Palestina. Alieleza kwa uzito na majonzi kuwa; siku hii ya leo ambayo ni Ijumaa ya mwisho katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, Kiongozi wa kiroho wa Waislamu, Imaam Khomein (ra), aliitangaza rasmi kwamba Ijumaa ya mwisho ya Ramadhani iwe ni siku ambayo Waislamu wote pamoja na wapenda amani, uhuru na haki duniani watoke hadharani na kupaza sauti zao dhidi ya dhulma wanazofanyiwa Wapalestina, huku wakibeba ujumbe mzito wa haki katika fikra na nyoyo zao.

Nukta ya kwanza, ambayo aliielezea ilikuwa ni kuwakumbusha Waislamu na Waumini wote kwamba; Qibla chao cha kwanza na Msikiti wao wa kwanza kabla ya kuelekea Masjidil-Haraam ilikuwa ni Masjid Al-Aqsa uliopo Palestina. Aliendelea kusisitiza kwa huzuni na tahadhari kwamba; hali ya Msikiti huo kila siku inazidi kuwa mbaya na hatarishi, huku mazingira yake yakizidi kuwa ya kutisha. Hivyo tunatoka tukiwa na lengo la kuwakumbusha Waislamu wasije wakausahau Msikiti wao na Qibla chao cha kwanza, kwani kusahau ni sawa na kupoteza sehemu ya historia na utambulisho wao wa kiimani.

Katika muendelezo wa khutuba yake Sheikh Jalala alisema; kuwa nukta ya pili iliyowafanya watu watoke katika siku hii ni kukumbushia kadhia ya wanaodhulumiwa duniani. Alisema kuwa leo hii mambo yanayojiri katika nchi nyingi duniani ni dhulma na ukandamizaji wa waziwazi. Mambo yanayojiri katika ardhi ya Palestina, Ghaza, Lebanon, Iraqi na sehemu mbalimbali duniani yanaonesha wazi kwamba dhulma na kumwaga damu za watu wasio na hatia vimekuwa jambo la kawaida katika ulimwengu huu, jambo linaloumiza mioyo ya watu wenye huruma na ubinadamu.

Nukta ya tatu, ni kuhimiza mshikamano na umoja kati ya Waislamu wote duniani. Alieleza kuwa; jambo hili ni miongoni mwa mambo muhimu ambayo Imaam Khomein (ra) alikuwa akiyasisitiza sana. Imaam Khomein (ra) alikuwa akihimiza Waislamu wote waungane na kuwa kitu kimoja, wakiwa na sauti moja katika kusimamia haki na kadhia ya Wapalestina, kwani umoja wao ndio nguvu yao kubwa zaidi.

Nukta ya nne, ni kuukumbusha ulimwengu kwamba amani ni kitu muhimu sana hapa duniani. Hivyo basi, moja ya falsafa kuu ya Siku ya Qudsi ni kutangaza amani duniani. Ni kuhakikisha kwamba dunia inabakia kuwa sehemu ya amani na watu wanaishi kwa utulivu na heshima ya utu wao. Leo hii tunaona jinsi amani ilivyopungua na kutoweka katika maeneo mengi ya ulimwengu, hivyo tunatoka kwa sauti ya pamoja kushinikiza kwamba, yale yote yanayoendelea ulimwenguni yasitishwe na kila mmoja apewe haki yake, kwa sababu sote tuna haki ya kuishi kwa amani na heshima.

Nukta ya mwisho, ni kukumbusha utu na ubinadamu. Sheikh Jalala alieleza kwa masikitiko kuwa; mambo yanayofanyika leo duniani yanaonesha wazi kwamba utu na ubinadamu vimesambaratika katika ulimwengu huu. Hivyo basi, siku hii ni siku maalumu ya kuikumbusha dunia thamani ya utu, huruma na ubinadamu, ili watu warejee katika misingi ya haki na huruma.

Mwisho wa khutuba yake, Sheikh Hemedi Jalala aliomba dua kwa unyenyekevu na uongofu wa moyo kuwaombea Waislamu wote duniani, hasa watu waliodhulumiwa wa Palestina, huku akimuomba Mwenyezi Mungu awape subira, nguvu na hatimaye ushindi wa haki juu ya dhulma.

Siku ya Qudsi ni siku ya kutangaza amani duniani

Siku ya Qudsi ni siku ya kutangaza amani duniani

Siku ya Qudsi ni siku ya kutangaza amani duniani

Siku ya Qudsi ni siku ya kutangaza amani duniani

Siku ya Qudsi ni siku ya kutangaza amani duniani

Siku ya Qudsi ni siku ya kutangaza amani duniani

Siku ya Qudsi ni siku ya kutangaza amani duniani

Siku ya Qudsi ni siku ya kutangaza amani duniani

Siku ya Qudsi ni siku ya kutangaza amani duniani

Siku ya Qudsi ni siku ya kutangaza amani duniani

Siku ya Qudsi ni siku ya kutangaza amani duniani

Siku ya Qudsi ni siku ya kutangaza amani duniani

Siku ya Qudsi ni siku ya kutangaza amani duniani

Siku ya Qudsi ni siku ya kutangaza amani duniani

Siku ya Qudsi ni siku ya kutangaza amani duniani

Siku ya Qudsi ni siku ya kutangaza amani duniani

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha